Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Majalis za Muharram Zinaendelea kufanyika katika Mji wa Bukoba kwenye vituo vya Taasisi ya Kiislamu ya S.D.O ambavyo ni: Nshambya Center - Bukoba Mjini, Kemondo, Katobago, Muleba n.k). Majlisi hizi zinaendelea kwa muda wa Siku 12 za Mwezi wa Muharram katika kuhuisha Mapinduzi ya Imam Hussein (as) na kutoa mafunzo mbalimbali kwa Jamii ya Kiislamu yaliyomo ndani ya Harakati ya kihistoria ya Imam Hussein (as) iliyotengeneza Mapinduzi Makubwa yanayoendelea kutoa matunda yake hadi Leo hii.
29 Juni 2025 - 23:58
News ID: 1703088
Your Comment